Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amekamata magari 10 makubwa kwenye eneo la Usa River Arusha akidai kuwa huenda magari hayo yakawa yana hujumu uchumi wa Bandari ya Dar es salaam kwa maana ya kukwepa kulipa kodi.

”Nataka kujua magari haya yametoka wapi na je yanapita kihalali katika eneo langu, kazi niliyotumwa ni hii na hayo ndio mambo ambayo nilitakiwa niyafanye” Muro.

Muro amesema hayo kutokana na kukamata nyaraka ambazo zimefungwa kwa maana ya kuwa hazijawahi kufunguliwa kwa ajili ya kukaguliwa na kupelekea kuonekana kwamba magari hayo yamepita katika bandari ya Namanga ambayo ni ruti ndefu bila kukaguliwa.

”Tangu haya magari yametoka boda labda hayajahakikiwa na hakuna mtu amejisumbua kusimamisha na kuyakagua amesema kuwa magari hayo tangu yatoke boda hajahakikiwa, na njia nyepesi ya kutoka Dar es salaam sio Namanga, Namanga ni ruti kubwa sana kwahiyo nalo pia likatuongezea mashaka …..je hizi ni zilezile jitihada za kuhujumu bandari yetu ya Dar es salaam na kama ndio basi si kwa Arumeru lengo letu ni kuhakikisha tunalinda biashara zetu lakini pia tunalinda uhusiano wetu na nchi jirani” amesema Muro.

Aidha Muro amesema hawezi kuruhusu uhujumu wa aina hiyo utokee wilayani kwake hivyo ameyakamata magari hayo kuhakiki endapo yamepitia taratibu zote za uvukaji boda au wameenda kinyume na sheria.

David Silva afuata nyayo za Iniesta, Pique
Wabunge mbaroni kwa kushambulia gari la Rais