Imewekwa rasmi Septemba 1, mwaka huu msanii toka Tanzania Naseeb Adbul, maarufu kama Diamond Platinumz kafanya kazi nyingine mpya na msanii toka Nigeria, Patoranking kwenye wimbo wake unaenda kwa jina la ‘Love you die’.

Love you die ni wimbo unaofanya vizuri katika playlist ya nyumbo za Youtube Tanzania, ambapo kwa sasa imeshika nafasi ya nne katika nyimbo zinazotazamwa na kufanya vizuri, ambapo nafasi ya kwanza ikiendelea kubuluzwa na Alikiba na kibao chake cha Seduce me, nafasi ya pili ikiendelaea kushikwa na wimbo kutoka WCB, Zilipendwa.

Tangu wimbo huo uwe hewani umepata watazamiaji 294, 370 ndani ya muda mchache, ndio sababu iliyofanya ipande nafasi nzuri katika nyimbo zinazotazamwa zaidi.

Patoranking alitumia kurasa yake ya Instagram kuzima tetesi zilizozagaa hapo awali kuwa anatarajia kupata mtoto kama ambavyo watu walidhani kutokana na baadhi ya picha alizokuwa akizipost kabla hajaweka wazi ujio wa wimbo wake mpya aliofanya na Diamond Platinum.

Hapa chini tazama video ya wimbo huo.

Harry Kane amaliza ukame wa mabao Uingereza ikishinda dhidi ya Malta
Video: Demokrasia Kenya ilivyoshangaza dunia