Kufuatia kipindi cha Mkasa kinachofanywa na chombo cha habari cha Dar24 ambacho kilimuibua kijana Hamad Awadh mwenye umri wa miaka 28 ambaye anatumia mashine ya umeme kupumua mara baada ya mapafu yake kusinyaa na moyo wake kuhama, Shirika la Umeme Tanzania limeamua kumsaidia kijana huyo kwa kuchukua hatua za kumuwekea umeme.

Kaimu Meneja Mawasiliano Tanesco, Leila Muhaji amesema wameanza kufanya mchakato wa kufunga umeme nyumbani kwa kijana huyo ili uweze kumsaidia kuendelea kupumua kwa kutumia mashine zake ambazo zinatumia nguvu ya umeme au gesi.

Hivyo mapema leo hii mafundi waliwasili nyumbani kwake kuangalia namna ambavyo wanaweza kufanya kumfungia umeme kijana huyo.

Mbali na hatua hizo, Jopo la madaktari mabingwa wa 5 wa kifua, mapafu na magonjwa mengine ya kuambukizwa kutoka hospitali ya taaluma na tiba ya Mloganzila na Muhimbili wamekutana na kufanya tathmini kubaini kwa kina ugonjwa unaomsumbua ili waweze kumtibu kijana huyo.

Mamia wamlilia aliyewahi kuwa Waziri wa mambo ya Nje
Madee kufuta nyimbo alizofanyia Afrika Kusini