Mshambuliaji mpya wa klabu ya Arsenal Alexandre Lacazette jana usiku alikuwa shujaa wa ‘Emirates Stadium’ baada ya kuisaidia klabu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya West Bromwich Albion katika mchezo wa Ligi kuu ya Uingereza kwa kupachika bao dakika ya 20 kipindi cha kwanza na bao lingine dakika ya 67 kipindi cha pili alilofunga kwa njia ya penati.

Alexandre Lacazzete mpaka sasa amevunja rekodi ya Brian Marwood iliyowekwa mwaka 1988 ya kufunga katika michezo mitatu ya mwanzo ya ligi ya EPL.

Matokeo hayo yanawafanya Arsenal kubaki katika nafasi ya saba ya msimamo wa ligi kuu Uingereza wakiwa na alama zao 10 huku Manchester City wakiwa kileleni.

Tazama magoli yaliyofungwa na Lacazette hapa chini;

Video: Daktari aeleza Manji alivyo hatarini kupoteza maisha, Sakata la Lissu lilivyomuibua Nyalandu
Magazeti ya Tanzania leo Septemba 26, 2017