Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimezindua Ripoti ya Haki za Binadamu ya mwaka 2017 kwa Tanzania Bara
Ripoti hiyo imesheheni maelezo kamili ya hali halisi ya haki za binadamu ikionyesha uvunjifu na ulinzi wake huku ikibeba dhana kuu ya “Watu Wasiojulikana” Tishio la Haki za Binadamu.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa kituo hicho, Hellen Kijo Bisimba amesema kuwa ripoti hiyo ni mtazamo wa haki za kiraia na kisiasa ya mwaka 2017, iliyoandaliwa na LHRC na ZLSC inaonyesha kwamba haki hiyo inaminywa, hasa kwenye kujadili masuala ya kisiasa na kupelekea kuvunja haki ya kushiriki katika masuala ya kisiasa