Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ameipongeza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kutenda haki ya kumfutia mashtaka, Juvenile Donald Shirima aliyekuwa amefunguliwa kesi ya makosa ya mtandaoni.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam mara baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumwachia huru kijana huyo ambaye januari mwaka huu alikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kesi hiyo mara ya baada ya kuposti mtandaoni kilichokuwa kikimsibu mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema alipokuwa Gerezani.

“Niwape taarifa nzuri leo, maana kila siku inchi yetu imekuwa na taarifa mbaya, naipongza sana mahakama kwa kutenda haki ya kumwachia kijana huyu, kwani waliomfungulia kesi wameingia mitini na mafaili, kijana kapoteza muda mwingi wa masomo, hivyo kwa sasa ngoja akaendelee na masomo halafu mengine yatafuata,”amesema Lissu

Hata hivyo, ameongeza kuwa watu wengi sana wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka ya makosa ya mtandaoni hivyo kwa kufanya hivyo ni kukandamiza uhuru wa kutoa maoni ya watu.

 

Kalemani apiga marufuku uagizwa wa nguzo za umeme nje ya nchi
Ufaransa yatoa msaada wa Euro 250,000 kwa wakimbizi