Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amefunguka kwa kuwataka wakuu wa vyombo vya usalama nchini wawaelekeze watumishi wao kazi za kufanya na siyo kupoteza muda na rasilimali za nchi.
Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amemtaka Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Kamanda Modestus Francis Kipilimba na Mkuu wa Majeshi Tanzania, IGP Simon Sirro kuwapa uweledi mzuri wa kufanya kazi vijana wao.
“Wale vijana wenu ambao mmekuwa mkiwatuma wanifuate kila nilipo kwa kipindi cha wiki tatu sasa, jana nimefanikiwa kuwakaba kanisani St. Peters. Hivyo wakubwa hawa wa vyombo vya usalama wawaelekeze watumishi wao namna ya kutumia muda na rasimali ya nchi hii,”amesema Lissu
Hata hivyo, kwa upande mwingine, Lissu amemtaka Kamanda Sirro pamoja na Kamanda Kipilimba kupamba na wahalifu na wamuachie yeye kazi ya kuwajibisha walioko madarakani kwa mujibu wa sheria za nchi