Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amewataka wakuu wa wilaya kutoendelea na tabia ya kuwaweka ndani hovyo wananchi.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais Dkt. Magufuli ipo kwaajili ya kuwatumikia wanyonge na si kuwanyanyasa.

“Unajua si tu kwamba mkuu wa wilaya akiulizwa swali lenye changamoto anaamuru mtu awekwe ndani, muda mwingine mmepishana tu kidogo kauli anaamuru awekwe ndani, hapana hii haikubariki hata kidogo, kuna taratibu za kufuata sio kukurupuka tu,”amesema Kangi Lugola

Hata hivyo, amelitaka jeshi la polisi kujiridhisha kwanza kwa kuchukua maelezo kwa mhusika kabla ya kumuweka ndani mtu yeyote kwa amri ya mtu fulani.

 

Video: Costech kuwarahisishia Watanzania usomaji machapisho
Mtawa afariki dunia baada ya kujirusha kutoka Ghorofani