Wakulima wa mkoani Tanga huko Lushoto sasa wameanza kuneemeka kufuatia kupata masoko ya uhakika kupitia kampuni ya MacLeans BeneCIBO iliyoamua kuwakomboa wakulima kwa kununua mazao tangu yakiwa shambani.
Issa Khalifa ambaye ni mkulima wa mbogamboga toka Lushoto ameeleza kinagaubaga namna ambavyo alianza kukata tamaa ya kufanya kilimo kutokana na changamoto kubwa ya masoko inayowakumba wakulima wengi hapa nchini.
Tangu ujio wa MacLeans BeneCIBO ambao wameamua kwenda bega kwa bega na wakulima, Issa anasema hii imewapa nguvu ya kurudi tena mashamabni na kufanya kazi kwa juhudi zote kwani sasa uhakika wa masoko upo wa kutosha.
”Kipindi cha nyuma kidogo nilikuwa nakata tamaa na kilimo kutokana na changamoto nyingi nilizokuwa nazipata mojawapo ya changamoto ilikuwa ni changamoto ya masoko unaweza ukalima kipande chako halafu ukakosa sehemu ya kuuzia” amesema Issa.
Ameongezea ”Lakini sasa nina muhamko kutokana na uhakika wa masoko hasa hawa wa BeneCibo ambao wanakuhakikishia kabisa soko lako”.
Tazama Video hapa chini.