Madaktari kutoka nchini India wamewasili nchini kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali za kiafya huku wakitarajiwa kutoa elimu kwa baadhi ya wataalamu wa sekta hiyo hapa nchini.
Aidha, ujio wa madaktari hao ni moja ya mikakati ya kudumisha mahusiano kati ya India na Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiafya, biashara na utamaduni.
Madaktari hao watatoa huduma zao kupitia hospitali ya Aga Khani hivyo watu wanaosumbuliwa na matatizo mbalimbali wameombwa kufika hospitalini hapo.
Ujumbe huo wa madaktari umewasili nchini juzi kwa ajili ya kuweza kutoa huduma mbalimbali za kiafya kwa lengo la kupunguza idadi kubwa ya wagoanjwa ambao wamekuwa wakitumia gharama kubwa kusafiri kwenda kupata matibabu nje ya nchi.