Umoja wa Madereva wa Mtandaoni Tanzania (TADO) wanaendelea na mgomo wao wa saa 48 wakiitaka Kampuni ya Uber kusikiliza malalamiko yao kwani wamechoka kuendelea kukandamizwa kila iitwapo leo kwa kufanya kazi ambayo haina faida.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Katibu wa Umoja huo, Fredy Peter alipokuwa akizungumza na Dar24 Media ambapo wameilalamikia Uber kwa kuwalipa asilimia ndogo huku ikilazimisha makapuni mengine kupunguza asilimia hali inayopelekea kipato cha madereva kushuka na kushindwa kujikimu kimaisha.

“Hii kampuni ya Uber imeleta matatizo makubwa badala ya kuleta fursa kwa watanzania,” amesema Peter

Aidha, Peter amesema kuwa wapo kwenye hatua za kusajili umoja wao ili wajiunge na Shirikisho la Madereva Nchini (TDF) ili waweze kupata mtetezi atakaye wasimamia na kuwasaidia katika kuwaondolea changamoto mbali mbali zinazowapata katika kazi yao.


Breaking News: Huu ndiyo uamuzi wa MBOWE kuhusu CHADEMA muda huu

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Septemba 20, 2018
Video: Mbowe afanya maamuzi magumu Chadema