Gari la polisi lililokuwa limebeba mahabusu jana lilipata ajali eneo la Kenyata Jijini Mwanza kwenye mzunguko wa samaki na kusababisha mahabusu mmoja na askari kupata majeraha

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi  Mkoani Mwanza Naibu Kamishna, Ahmed Msangi ambapo amesema kuwa Gari hilo lenye namba za usajili PT 3643 aina toyota land cruiser pick up lililokuwa limetoka mahakama ya wilaya ya Nyamagana, lilikuwa limewabeba mahabusu waliokuwa wanarudishwa gereza la butimba na ghafla lilipofika eneo la mzunguko wa samaki gari namba T 230 BMP aina ya toyota vitz.

“Madereva wengi wana dharau na ndiyo maana ajali kama hizi huwa zinatokea. kwa hili lilotokea lingeweza kusababisha matatizo makubwa mno kwani askari wetu walikuwa wapo na silaha nzito na mahabusu waliokuwa wakisindikizwa walikuwa hatari kwani wangeweza kuumia au kupata fursa za kukimbia na ukizingatia askari walikuwa na silaha yangetokea mengine makubwa,”amesema Kamanda Msangi

Jaji Lubuva akerwa na kauli za wanasiasa
Video: Hii ni laana na unyama kuhujumu uchumi wa nchi- Dkt. Mpango