Siku ya October 6, 2016 ilisambaa video kwenye kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha mwanafunzi, Sebastian Chinguku wa shule ya kutwa ya Sekondari, Mbeya akipigwa kwa mateke na makofi na Walimu ambao walikua kwenye shule hiyo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo. Kufuatia tukio hilo Serikali imechukua hatua mbali mbali kwa walimu waliohusika ikiwa ni pamoja na kumvua madaraka mkuu wa shule hiyo kwa kufumbia macho kitendo hicho lakini pia imewachukulia hatua walimu wahusika wa kitendo hicho.

Mwalimu Frank Msigwa ni kati ya walimu waliotajwa kuhusika na kitendo hicho ambapo amedai kuwa yeye siyo chanzo cha tukio hilo na hahusiki. Msikilize hapa kwenye hii video.

Baraza la mitihani kuanza kufanya uhakiki wa vyetu kwa watumishi wa Serikalini
DRC Yamponza Javier Clemente, LFF Yamfungashia Virago