Taasisi ya Imamu Bukhari imelalamikia utaratibu uliowekwa na Askari Magereza wa kuwahudumia Masheikh wa uamsho wanaoshikiliwa kwa kosa la kujihusisha na ugaidi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sheikh Khalifa Khamis alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,amesema kuwa utaratibu wa kutoa huduma kwa masheikh hao.
“Tunasikitishwa sana na jinsi watu hawa wanavyotendewa utadhani kama sio Watanzania, sasa tunajua hata rais Dkt. Magufuli hajui kinachoendelea, inasikitisha sana ndio maana tumeamua kuliweka hadharani ili kila mtu aelewe kinachoendelea,”amesema Sheikh Khamis.
Hata hivyo, ametaja orodha ya watuhumiwa wa ugaidi katika mikoa yote hapa nchini na kuiomba Serikali kutolea maamuzi kesi hizo kwani watuhumiwa hao wamekaa kwa muda mrefu Magerezani.