Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amekabidhi pikipiki 49 kwa vijana wa wilaya ya Ruangwa ili waweze kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.

Majaliwa amekabidhi pikipiki hizo baada ya kumaliza kuhutubia wananchi kwenye uwanja wa shule ya msingi Likangara, ambapo amewataka vijana hao kuhakikisha wanakuwa waaminifu kwa kufanya kazi kwa bidii ili pikipiki hizo ziwe na tija.

Amesema vijana wanaoendesha pikipiki maarufu bodaboda wanatakiwa kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali.

“Ukiendesha pikipiki lazima uhakikishe kwamba una leseni, bima, vaa kofia ngumu wewe na abiria wako na marufuku kubeba abiria zaidi ya mmoja.”

 

Kesi ya Masogange yapigwa kalenda
DCI amsaka aliyesambaza video mchele wa plastiki