Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa wiki moja kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe kumpa maelezo kuhusu sababu za Tanzania kutokukamilisha mkataba wa Mawakili wa Afrika Mashariki kutambuana katika utendaji wao.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo Novemba 25, 2016 wakati akimuwakilisha Rais Dk. John Magufuli katika ufunguzi wa mkutano wa 21 wa mwaka wa Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

“Nimeshtushwa kidogo kusikia kwenye taarifa yenu kuwa mkataba huo uliolenga nchi zote za Afrika Mashariki hautaihusisha Tanzania kutokana na kutokukamilisha sehemu yao ya kuufanyia kazi, nitahitaji maelezo,”

“Nitapenda kupata maoni yako wewe mwenyewe mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania kwa vile wewe ni Mwanasheria mwandamizi na siyo Mwanasheria  wa Tanganyika Law Society peke yake kwa nini Tanzania haijakamilisha mkataba huu,” – Majaliwa

 

Aliyemwambia ‘mteja’ ataisoma namba kwa kumchagua Magufuli abanwa
TPSF yaiomba Serikali kuboresha sera ya wajasiriamali