Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amempongeza mwanamasumbwi wa Kitanzania, Hassan Mwakinyo kwa kumchapa bondia Mwingereza, Sam Egginton.

Mwakinyo alimchapa Egginton kwenye raundi ya pili ya pambano lao la masumbwi lililofanyika Jumapili, Septemba 9, 2018, huko Birmingham nchini Uingereza.

Majaliwa ametoa pongezi hizo leo Septemba 14, 2018 wakati akiahirisha mkutano wa 12 wa Bunge, Bungeni jijini Dodoma. Bunge limeahirishwa hadi Novemba 6, 2018.

Amesema bondia huyo amelipa Taifa heshima kubwa kwa kulitangaza kimataifa katika nyanja ya michezo, hivyo amewataka wanamichezo wengine nchini waige mfano wake.

Mwandishi aliyepotea apatikana akiwa hoi
Serikali yatumia bilioni 216 kukamilisha mradi wa Umeme