Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majliwa ametia saini kitabu cha maombolezo na kumpa pole Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kangi Lugola kufuatia kifo cha mke wake, Kamishna Msaidizi wa Polisi Mary Lugola Jijini Dar es salaam.

Kamishna Msaidizi wa Polisi, Mary Lugola alifariki dunia Januari 1, 2018 katika Hospitali ya Rabininsia Jijini Dar es samaam alipokua akipatiwa matibabu.

 Hadi umauti unamkuta Marehemu Mary Lugola alikuwa Afisa Mnadhimu Kikosi cha Polisi Reli nchini. Mwili wa marehemu Mary Lugola utasafirishwa kesho kwenda Mkoani Mara kwa mazishi.

IGP Sirro akagua magari 119 ya Jeshi hilo bandarini
Picha: Samia Suluhu ahudhuria msiba wa mke wa Kangi Lugola