Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Januari Makamba, na Mkurugenzi Mkuu Shirika la Kimataifa la Mazingira Duniani (UNEP), Erick Solheim,wametembelea kikundi cha wakina mama kinachojuhusisha na uzaaji wa mkaa kilichopo Ubungo Jijini Dar es salaam.

Makamba amesema wameamua kumtembeza kiongozi huyo ili ajionee shughuli za mkaa zinavyofanyika hapa nchini ili waweza kushirikiana nao kuona namna ya kuweza kupunguza matumizi ya mkaa na kuwawezesha wakina mama kufanya shughuli zingine za kuwapatia kipato.

Amesema kuwa jitihada za nchi za kupunguza matumizi ya mkaa zinahitaji ushirikiano na Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa.

“Ukataji wa mkaa umeongezeka sana kiasi kwamba,nchi yetu inatishio la kutokea jagwa hivyo tunataka tutokomeze kabisa tatizo hili,”amesema Makamba.

AFCON 2017: Algeria Yatupwa Nje
Video: Mkurugenzi wa mazingira Duniani, Waziri Makamba watembelea Dampo