Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, huku baadhi ya mawaziri wakimwagwa na wengine kuendelea na nafasi zao.

Mawaziri walioendelea na nafasi zao ni pamoja na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyeyembe.

Katika baraza hilo jipya walioahwa ni pamoja na Dkt. Jumanne Maghembe na Naibu wake Ramo Makani ambao walikuwa Wizara ya Maliasili na Utalii huku aliyekuwa Naibu Waziri wa Tamiseni Seleman Jafo akiukwaa uwaziri wa kamili wa wizara hiyo.

Aidha, wengine wapya walioukwaa uwaziri kamili ni pamoja na aliyekuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina ambaye amekuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

Video: Kashililah ang'olewa Ukatibu wa bunge
Selasini na wapiga kura wake kuamua kuhusu Ben Saanane