Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya ziara ya ukaguzi wa miundombinu na mazingira Jijini Dar es salaam.
Katika ziara hiyo, Makamu wa Rais amewataka wananchi Jijini Dar es salaam kutunza mazingira na kuepuka kutiririsha maji taka katika mitaro iliyojengwa ili kuweza kuepuka mlipuko wa magonjwa.
Amesema kuwa kama wananchi watashirikiana kutunza mazingira, basi watakuwa wamesaidia kuondokana na majanga ambayo yanaweza kujitokeza.
“Mitaro mingi imekuwa ikijengwa, lakini wananchi wamekuwa wakibadili kuwa dampo la takataka, lakini jingine ni utiririshaji wa maji machafu, kitu ambacho si cha kisitaarabu,”amesema Samia Suluhu