Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwa ameambatana na Mstahiki Meya wa jiji, Mameya wa Halmashauri na Madiwani wamefanya ziara Mkoani Morogoro kwenye Stendi Mpya ya Mabasi ya Msamvu kujifunza namna stendi hiyo imefanikiwa kuweka mazingira jumuishi kwa makundi yote wakiwemo wafanyabiashara na wasafiri.
Makonda amesema kuwa Dar es salaam ipo katika hatua ya ujenzi wa stendi mpya ya kisasa Mbezi Luis itakayogharimu zaidi ya shilingi Billion 50.9 ambayo itakuwa na ukubwa mara nne ya Stendi ya Msamvu ambapo itakuwa na uwezo wa kupokea mabasi 500 kwa wakati mmoja.
Aidha. RC Makonda amesema kuwa Stendi mpya ya Mbezi Luis itakuwa na Jengo la Abiria,Utawala, Maegesho ya mabasi, shopping mall, Hotel, Taxi, Bajaji, Pikipiki, Benki, Petrol station, Apartment, ofisi za mabasi, sehemu ya wafanyabiashara, mama Lishe, Vyoo, kituo cha polisi na sehemu ya kuhifadhi mizigo.
Kwa upande wa viongozi wa Mkoa wa Morogoro wameshukuru kupokea ugeni huo mzito na wamesema kuwa watafika Dar es salaam kujifunza mambo mengi ambayo Jiji hilo limepiga hatua na kupata sifa kubwa ndani Na nje ya nchi.