Mradi wa Ujenzi wa Mabweni unaosimamiwa na Wakala wa Ujenzi Tanzania (TBA), uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam unatarajiwa kukamilka hivi karibuni.

Hayo yamesemwa mapema hii leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi katika mradi huo.

Amesema kuwa kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa mabweni hayo kutapunguza gharama kubwa ambayo wamekuwa wakiipata wanafunzi wa chuo hicho kupanga vyumba mitaani,

Aidha, Makonda ameongeza kuwa anajisikia fahari kubwa kufanya kazi chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwa anatimiza ahadi zake za kukamilisha Miradi mbalimbali katika Jiji la Dar es salaam ukiwemo mradi wa ujenzi wa mabweni hayo ya wanafunzi katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam.

Hata hivyo, Mabweni yanatarajiwa kuchukua zaidi ya wanafunzi 3840 kwa gharama nafuu.

 

Magazeti ya Tanzania leo Aprili 15, 2017
JPM alaani mauaji ya Polisi 8 Pwani