Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda amefanya ziara ya kukagua miundombinu iliyoathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua zilizonyesha siku chache zilizopita na kupelekea uharibifu mkubwa wa miundo mbinu.
 
Katika ziara hiyo ameambatana na Kamati ya Maafa ya Mkoa ambapo wametembelea maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na mvua ikiwemo eneo la Jangwani, Daraja la Malecela, Daraja la Korongo, Daraja la Tandale kwa Mtogore, Africana na Boko Basihaya na kutoa pole kwa wahanga wa mafuriko hayo.
 
Aidha, Makonda amewataka wananchi waliojenga kwenye maeneo hatarishi kuchukuwa tahadhari mapema kwakuwa wataalamu wa hali ya hewa wametangaza kuwa mvua kubwa zitaendelea kunyesha.
 
Amesema kuwa ujenzi wa miundombinu iliyoharibiwa ikiwemo ya Maji, Umeme, Mitaro, Barabara na Madaraja inaendelea kukarabatiwa ili huduma za kijamii ziendelelee kupatika kama ilivyokuwa hapo awali

Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 29, 2017
Yanga, Simba zatoka suluhu huku Kichuya akiweka rekodi ya aina yake