Chama cha wamiliki wa malori ya mchanga jijini Dar es salaam kimesema kitatoa huduma ya kubeba mchanga bure katika ujenzi wa ofisi za walimu 402 ndani ya Mkoa wa Dar es salaam ili kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika uwaletea wananchi maendeleo
Aidha, kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amepokea msaada huo na amewashukuru wamiliki wa malori na kuwataka wadau wengine waige mfano kwa kuwa jambo linalofanyika ni kwaajili ya kuiboresha sekta ya elimu huku akisema hatua hiyo itakwenda kuchochea maendeleo ya elimu ndani ya mkoa wa Dar es salaam.
“Nawashukuru sana kwa sababu mmenifanya niendelee kutembea kifua mbele na kupata usingizi, hiki kitu ambacho mmekifanya nikikubwa sana kwa mkoa wa Dar es salaam, kina manufaa kwa elimu yetu kwa ujumla, kwahiyo mimi niwashukuru kwa hatua hiyo pia wadau wengine watuunge mkono kwa sababu kama tumemaliza suala la mchanga bado kuna maeneo mengine kwenye mradi huu ambayo yanahitaji pesa,” amesema Makonda