Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo Oktoba 11, 2016 amesema kuna mradi mkubwa unaoendelea Chanika wilaya ya Ilala, Dar es salaam wenye thamani ya shilingi bilioni 8.8. Makonda ameutaja mradi huo kuwa ni jengo kubwa la hospitali ya akina mama lenye nyumba za kuishi madaktari pia sehemu ya kusomea masomo ya ukunga. Mradi huo ni moja kati ya miradi mingine ambayo imezindulkiwa leo na Makamu wa Rais, samia Suluhu.

Makonda ametoa shukrani za dhati kwa AMSONS Group ambao wamejitolea kujenga na kuusimamia kikamilifu miradi hiyo inayotarajiwa kukamilika ndani ya miezi kumi na mbili na kukabidhiwa kwa Paul Makonda.

Obama amvaa Trump, amchongea kwa chama chake
Samia Suluhu azindua mradi wenye thamani ya shil. bil. 4.5