Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  amesema kuwa anatarajia kuunda Kamati ya Wanasheria Waliobobea kwa ajili ya kuwasaidia wakina mama wanaopewa ujauzito na kukataliwa na wanaume wao na kusababisha kukosekana kwa huduma na malezi bora.

Ameyasema hayo katika hafla ya kukabidhi Mashine za Ultra sound kwa vituo vya afya na hospitali 10 ambazo zimeonekana kutoa huduma bora za ya uzazi na mtoto.

Aidha, Makonda amesema kuwa baadhi ya wanaume wamekuwa wakiwatelekeza wakinamama baada ya kuwapa ujauzito bila kuwapa matunzo, hivyo amepanga kuunda jopo la wanasheria watakaowashughuliki wanaume hao.

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 17, 2017
Tume ya uchaguzi yapokea taarifa kutoka kwa Spika Ndugai