Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa kukatika kwa umeme imekuwa ni kero kubwa kwa wananchi wa jiji la Dar es salaam na wakati mwingine kusababisha hasara hivyo anaamini TANESCO ya sasa chini ya  Serikali ya awamu ya Tano itamaliza kero hizo.
Ameyasema hayo wakati wa kikao na viongozi wa Tanesco jijini Dar es salaam, ambapo wamemuahidi kuwa Umeme utaongezeka maeneo yote yaliyokuwa yakisumbuliwa na upatikanaji wa Umeme, hivyo hali itakuwa shwari.
Aidha, kuhusu suala la umeme mashuleni wamekubaliana kuandaa mchanganuo wa mahitaji yanayohitajika kisha kufikisha ofisini kwake ili kila shule iunganishwe na huduma ya umeme.

Magazeti ya Tanzania leo Novemba 3, 2017
Halotel watoa msaada wa simu kwa Jeshi la zimamoto