Katika kuhakikisha kuwa anaunga Mkono Jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameziagiza Manisapaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam kubadilisha Mfumo wa utoaji wa asilimia 10% kwa kina mama na vijana ili fedha hizo ziweze kuleta tija katika kutekeleza dira ya taifa.

Ameyasema hayo alipokuwa akizindua viwanda vidogo vidogo vya wajasiliamali Katika eneo la Mwananyamala Manispaa ya Kinondoni ili kuweza kuwasaidia wananchi hao ambao wamekuwa wakijitaftia ridhiki kwa njia halari ya kujiajiri.

Aidha, Makonda amesema kuwa katika kutekeleza Mpango huo ameamua kuzindua majengo yatakayotumika kwa ajili ya uanzishaji wa viwanda vingine vidogo vidogo katika eneo hilo ili kuweza kutoa wigo mkubwa kwa wajasiliamali wengine watakao ongezeka katika maeneo hayo.

Hata hivyo, Makonda amewataka wafanyabiashara ndogo ndogo kuanza kuuza bidhaa zinazozalishwa na wafanyabiashara wa ndani  ili kuweza kukuza na kupandisha thamani ya bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya Tanzania.

Tigo yawazuia Mwana FA, AY kuhudhuria tamasha la Fiesta
Messi apiga 'Hat-trick' Barcelona ikipaa kileleni