Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameahidi kuwapatia watumishi wa sekta za elimu, polisi na afya viwanja kwa ajili ya ujenzi wa makazi ya kuishi ili kutatua changamoto zinazowakabili katika kutoa huduma kwa wananchi.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa viwanja hivyo vitauzwa kwa bei nafuu ambapo kila square mita moja itauzwa kwa shilingi elfu nne tofauti na bei ya awali ya shilingi elfu kumi na tano.

“Kila mtumishi atakayefanya malipo ya awali ataruhusiwa kujenga huku akiendelea kulipa taratibu ambapo ataruhusiwa kulipa gharama hizo kwa muda wa miaka mitano,”amesema Makonda

Hata hivyo, Makonda amewaagiza wakurugenzi wa halmshauri wasiwalipishe watumishi hao vibali vya ujenzi ili kuwapunguzia gharama watumishi hao.

Mbunge Musukuma akamatwa na Polisi
Mambosasa: Tunaendelea kuwakamata wanaomuombea Lissu