Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewatangazia walemavu wenye mahitaji ya miguu katika mkoa wa Dar es salaam kujitokeza siku ya Agosti 14 na 15 kujiandikisha na kupimwa ili waweze kupatiwa miguu ya bandia itakayo wasaidia katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Makonda amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam, amesema siku hiyo kutakuwa na wataalamu (Madaktari) watakao chukua vipimo iliwawatengenezee miguu kulingana na mahitaji.
Makonda ameamua kuwasaidia wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama za vifaa hivyo, ambapo atawapatia miguu hiyo bure, kutokana na wananchi wengi waishio mkoa wa Dar es salaam kutokua na uwezo wa kumudu gharama za manunuzi ya miguu ya bandia pindi wanapopata ajari na kukatika miguu hali
“Nimefanikiwa, na namshukuru mwenyezimungu nimepata wadau ambao wamenipatia miguu hiyo itakayo wasaidia wananchi wangu mia mbili (200) kwa awamu ya kwanza ambapo watapatiwa miguu hii ya bandia na kuweza kutupa magongo yao na kurejea katika shughuli zao” Amesema Makonda.