Simba ni miongoni mwa wanyama ambao ni jamii ya paka, lakini pia ni wanyama ambao hupenda kuishi katika makundi makundi kifamilia kama ilivyo kwa binadamu, na familia zao huweza kuwa na simba takribani kumi na tano.

Njia rahisi ya kuwatambua kwa jinsia zao ni muonekano pamoja na majukumu, simba dume shingoni amejaa manyoya mengi, simba jike huwa na manyoya sawa mwili mzima.

Katika maisha yao ya kifamilia hugawana majukumu ambapo chakula hutafutwa na simba jike na awapo mawindoni jukumu la simba dume huwa ni kulinda mipaka yao ambapo simba humiliki eneo kubwa kuanzia mile 10.

Uhai wa simba kuishi ni kati ya miaka 10 mpaka 14 lakini kwa simba wa Afrika hufika hadi miaka 17, Simba huanza kufundishwa mbinu za uwindaji watoto wake tangu wakiwa wadogo kabisaa, ambapo huwatanguliza mbele na kuanza kuwabughuzi kwa kuwapiga piga ngwala, jambo ambalo hufanya watoto wake kuwa wenye hasira na wakali sana, na mbinu hizo ndio hutumia akiwa anawinda ukubwani.

Mambo mengine 6 usiyoyafahamu kuhusu Simba.

Faida 6 za kula mayai wakati wa kifungua kinywa
Video: Hii sio sahihi, nyie Wamachinga kuweni waaminifu- RC Makonda

Comments

comments