Manchester United wameibuka vinara wa kundi A kwa kuwa na alama 15, baada ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya CSKA Moscow, huku FC Basel nao wakisonga mbele kwa kuwa na alama 12 baada ya ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Benfica.

Katika kundi B Bayern Munich wamekiichapa Paris Saint Germain, goli 3-1 na Celtic wakafungwa 1-0 na Anderlecht hivyo PSG na Bayern ndio waliofuzu hatua inayofuata huku Celtic, wakishiriki michuano ya Europa ligi.

Aidha, katika kundi C, Atletico Madridi wameshindwa kusonga mbele baada ya kukubali sare ya goli 1-1 na Chelsea ugenini hivyo wanakwenda kushiriki Europa ligi.

Barcelona, wamemaliza hatua ya makundi bila ya kufungwa baada ushindi wa 2 – 0 dhidi ya Sporting CP, na kumaliza vinara kwa jumla ya alama 14, wakifuatiwa na Juventus wenye alama 11 baada ya kuwachabanga Olympiacos kwa mabao 2-0

Video: Mwinyi atua kwa Lissu, Wabunge tisa wa Ukawa watajwa kuhamia CCM
Mpina amwamuru mwekezaji kuondoka