Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),  limemwandikia barua msemaji wa Yanga, Jerry Muro ya kumtaka kufika katika Ofisi za TFF siku ya Jumamosi ya tar 2/7/016 kukutana na kamati ya maadili ili kutaka kujua kwanini amekua akipingana na shirikisho hilo la mpira wa miguu Tanzania.

Kufuatia hayo Katibu wa tawi la Tandale kwa mtogole,Waziri Jitu amejitokeza na kusema wanapinga maamuzi yote yanayofanywa na Rais wa TFF, Jamali Malinzi na kama yakifumbiwa macho yataua soka la Tanzania.

“Wamemuita msemaji wetu wa club, Jerry Muro na tunazo taarifa kuwa wanataka kumfungia miaka mitatu kutojihusisha na soka’’ – Jitu.

Mashakabiki hao wameitaka TFF kutokujaribu kumfungia msemaji wao kwani yeye kaajiriwa kwasababu ya mdomo na kama wakimfungia basi watakua wanahatarisha ajira yake na kazi yake ni kuongea na si kukaa ofisini kuchezea laptop.

Video: Mawaziri wa mambo ya nje Tanzania na Rwanda wakitiliana saini
Video: Rais wa Rwanda Paul Kagame azungumzia uhusiano wa Tanzania na Rwanda