Wafanyakazi za ndani wa kike kutoka nchini Tanzania waliopo  Oman na nchi za falme za Kiarabu UAE, wanafanyiwa vitendo vya kinyama huku wakidharirishwa kimwili na kingono,wakifanyakazi kwa masaa mengi huku wakilipwa mishahara midogo.

Ripoti iliyotelewa na Shirika linalojishughulisha na Haki za Binadamu,(HRW) imesema kuwa kuna maelfu ya wafanyakazi wa ndani kutoka Tanzania nchini Oman na UAE wamekuwa wakifanyakazi kwa masaa mengi huku wakilipwa mishahara midogo, kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch (HRW).

Watafiti wake waliwahoji wafanyakazi 50 kati yao na kugundua kuwa karibu wote walipokonywa pasipoti zao walipowasili na kulazimiswa kufanya kazi hadi masaa 21 kwa siku bila kupumzika.

Aidha, wafanyakazi waliodiriki kuwatoroka waajiri wao na mawakala wamesema kuwa polisi au balozi zao huwalazimisha kurudi la sivyo wangekosa mishahara yao hali iliyowachukua muda mrefu kutafuta pesa za kuwawezesha kurudi nyumbani.

Hata hivyo, wamesema kuwa hulipwa pesa kidogo kuliko zile walizokubaliana au muda mwingine kutolipwa kabisa na kupewa mabaki ya chakula kilichooza huku wakitukanwa na kudharirishwa kingono.

Takukuru yaanza kulifanyia kazi agizo la Dkt. Kigwangalla
Rais Buhari aunga mkono kufukuzwa kwa Walimu 20,000