Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ametoa onyo kali kwa wale wanaopanga maandamano, kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Ameyasema hayo hii leo Jijini Dar es salaam wakati wa kupokea vituo sita vya polisi vinavyo hamishika, ambapo amesema kuwa ni bora wakajikita katika kufanya kazi ili waweze kujiongezea kipato.

Amesema kuwa kwasasa kuna fursa kubwa ya viwanda, hivyo ni bora wakaitumia vizuri ili kuimarisha vipato na kujikwamua kimaisha.

“Ni vyema wakajikita katika kufanya kazi ili kuimarisha kipato kuliko kukaa na kuanza kuhamasisha maandamano,”amesema Masauni

 

Michael Richard Wambura apinga hukumu
Lissu atoa neno baada ya oparesheni ya 19