Mtayarishaji wa Muziki na mmiliki wa studio za Mazuu Records, Mazuu amemtambulisha msanii mpya kutoka jijini Nairobi nchini Kenya aitwae Rawbeena.

Mtayarishaji huyo ameiambia Dar24 kuwa msanii huyo mpya alilikuna sikio lake alipokuwa kwenye ukumbi mmoja wa starehe jijini Nairobi, baada ya kupewa nafasi ya kutumbuiza.

“Nilitembelea Nairobi katika moja ya kumbi za starehe ndipo nilipokutana na sauti nzuri ya mwanadada Rawbeena akifanya show. Nilivutiwa sana na sauti yake. Baada ya hiyo show nilimuita tukazungumza na mazungumzo hayo yalizaa matundo hadi nikamsaini kwenye lebo ya ‘Mazuu Records’,” alisema.

Tayari ameshaachia video ya wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Nipoze’, ikiwa ni mradi wa kwanza kutoka kwenye studio hizo.

Mazuu amesema kuwa mbali na video hiyo, wameshaandaa video 4 zilizoko tayari kuendeleza mashambulizi ya kuliteka soko. Amesema kuwa ‘Rawbeena’ ni kipaji kitakachofanya vizuri ingawa hiyo ndiyo project yake ya kwanza kufanya kwani nchini Kenya hakuwa ameshaanza kufanya kazi rasmi ya muziki zaidi ya kutumbuiza kwenye matamasha.

 

Basata Yamtosa Ney Wamitego
Watanzania wawili wapandishwa kuwa Marubani wakuu wa Fastjet