Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Taifa (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa chama chake hakitashiriki chaguzi zijazo.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa, haileti maana yeyote kushiriki chaguzi ambazo haziko huru.

Akizungumzia uchaguzi mdogo wa marudio uliofanyika katika Majimbo la Ukonga na Monduli, amesema kuwa katika majimbo hayo mawakala wa Chadema walikamatwa na kuzuiliwa na polisi.

“Huu uchaguzi wa marudio uliofanyika katika majimbo ya Ukonga na Monduli haukuwa huru, ndio maana sasa tumeamua kujitoa katika chaguzi zote zinazokuja ukiwemo wa jimbo la Liwale, hatutashiriki tena,” amesema Mbowe


Video: Mgomo wa Madereva wa Uber wazidi kutikisa, “Sisi siyo madereva wao, tumewapa masaa 48”

Video: Madereva wazidi kuwagomea Uber, wamlilia Rais Magufuli
Video: Hii ndiyo sababu ya kuoa mwanamke wa Kitanzania