Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni lililopo jijini Dar es salaam, Maulid Mtulia amesema kuwa ameamua kujiunga na chama cha mapinduzi CCM ili aweze kuwatumikia wananchi akiwa huru.

Ameyasema hayo wakati akikabidhiwa rasmi kadi ya chama hicho jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa sababu kubwa ya kuondoka CUF ni kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Dkt. Magufuli.

Amesema kuwa Rais Dkt. Magufuli alipokuwa akizindua ujenzi wa nyumba za Magomeni Kota alijitokeza na kuzungumza naye kuhusu maendeleo ya jimbo lake la Kinondoni, kitu ambacho kilionekana ni usaliti kwa upande wa upinzani.

Ufisadi wagubika mazishi ya Mandela
Facebook yawafungulia milango watoto kujiunga