Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Aida Khenani ameitaka Serikali kutatua changamoto ya ajira kwa vijana ambalo ni janga kubwa kwa wahitimu wengi wa vyuo vikuu.
Amesema kitendo cha vijana kukosa ajira wanajiona ni laana katika jamii.
”Idadi ya wahitimu wanaopatikana kwa mwaka kutoka kwenye vyuo mbalimbali haiendani na ajira inayotolewa kwa mwaka, vijana wengi wamelundikana mtaani, na kwa bahati mbaya sana mitaala yetu ya Tanzania inawatengeneza vijana wengi kuajiriwa sio kujiariri” Amesema Khenani.
Akizungumza hayo ametoa ushauri kwa serikali kuandaa mitaala itayomjenga kijana kuwa na uwezo wa kujiajiri zaidi kuliko kufikiria kuajiriwa.
Amekazia suala la kilimo kama njia mbadala ya ajira, japokuwa bado suala la kilimo halijapewa kipaumbele amesema bado kuna changamoto kubwa wakulima wanakumbana nazo.
Msikilize akitoa ushauri kwa Serikali ya Tanzania katika kuwajenga vijana kuwapa mbadala wa Ajira.