Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Rukwa Mheshimiwa Aida Joseph Khenani ameitaka serikali kutenga kiasi maalumu cha posho kwa ajili ya wenyekiti wa serikali za mitaa ambao hawalipwi posho na mishahara.
”Mimi mbunge nalipwa posho na mshahara, diwani analipwa posho na mshahara rais analipwa posho na mshahara kwa nini huyu ambaye ndiye msimamizi wa kwanza wa miradi halipwi” amehoji Mbunge Khenani.
Ameshauri Serikali iweke sheria za posho na zilipwe kwa mujibu wa sheria na sio kama ambavyo ipo sasa kwamba malipo ya mwenyekiti wa serikali za mitaa hutegemea makusanyo ya Halmashauri.
Amezungumza hayo kuelekea uchaguzi wa wenyeviti wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.
Bofya hapa chini kumsikiliza.