Mbunge wa Viti Maalumu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Neema Mgaya ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na kwa Watanzania wote kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere.

Akizungumza na Dar24 Media jijini Dar es salaam, Mgaya amesema kuwa ajali hiyo ni kubwa na imewafanya Watanzania kupoteza wapendwa wao.

“Napenda kutoa pole nyingi sana kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kwa Watanzania wote kwa ujumla kwa kupoteza ndugu zetu katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere huko Ukara, Ukerewe jijini Mwanza, kwakweli ni tukio la huzuni kweli kuwapoteza wapendwa wetu,”amesema Mgaya

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Septemba 27, 2018
TMA yatahadharisha kutokea kwa Mvua kubwa