Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee (Chadema) amesema kuwa sio lazima kuikubali bajeti ya Serikali hivyo wataendelea na msimamo wao bungeni wa kupiga kura ya hapana ili Serikali iweze kurekebisha pale inapokuwa na mapungufu.
Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi habari, amesema kuwa kambi rasmi ya upinzani bungeni itaendelea kupiga kura ya hapana katika bunge la bajeti mpaka pale Serikali itakakubaliana na maoni yao.
“Kupiga kura ya ndio au hapana ni haki ya mbunge, kwa hiyo kila mmoja ana uhuru wa kuamua lakini asilazimishwe, sisi tutaendelea kupiga kura ya hapana siku zote mpaka pale Serikali watakapotusikiliza,”amesema Mdee
Hata hivyo, ameongeza kuwa katika bajeti iliyopitishwa hivi karibuni kuna baadhi ya Wizara nyeti ambazo hazijapata fedha za kujiendeshea huku akiitolea mfano Wizara ya Kilimo ambayo imepata asilimia tatu.