Lionel Messi alifunga mabao manne na kuifanya Barcelona kuendelea kubaki kileleni mwa La Liga huku klabu hiyo ikiweka rekodiĀ  ya kushinda mechi zote msimu huu kwa kutoa kipigo cha mabao 6-1 dhidi ya Eibar.

Messi alifunga bao la kwanza daikika ya 20 kwa mkwaju wa penati na kuiweka Barcelona mbele kabla ya Paulinho kufunga la pili kwa kichwa dakika ya 38 kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kilianza kwa Barcelona kutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa na dakika ya 53 Denis Suarez alifunga bao la 3 kabla ya Sergi Enrich kuipatia Eibar bao la kufutia machozi dakika ya 57.

Lionel Messi akiwa katika ubora wake aliweza kupachika mabao matatu ndani ya dakika 28 akipiga bao la nne dakika ya 53, bao la tano dakika 62 na kupiga bao la 6 katika dakika ya 87.

Tazama video ya mabao hayo hapa chini;

Zari atoa ushauri na faraja kwa wanaosalitiwa
Nyalandu aweka kambi Nairobi kusubiri ruhusu ya kumpeleka Lissu Marekani