Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta, amewapa mwezi mmoja na nusu wafanyabiashara wa Mihogo katika fukwe za Coco, wawe wamehama na kupisha zoezi la ujenzi wa fukwe hizo unaotarajiwa kuanza Novemba 5, 2019.

Akizungumza na wafanyabiashara hao, Meya Sitta amewapa eneo jingine litakalokuwa karibu na sehemu yao ya awali na rahisi kufikiwa na wateja wao.

Hatatua hii imekuja ikiwa ni siku chache tu baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, aalipowaagiza  watendaji katika Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanaisimamiwa vyema miradi ambayo imekuwa ikisuasua.

Aidha baadhi ya wafanyabiashara katika eneo hilo wamesema kuwa eneo walilopangiwa kwenda kufanya biashara si rafafiki kwao, na kwamba eneo hilo hailina biashara kama ilivyokuwa hapo awali …, Bofya hapa kutazama

Philippe Coutinho afurahia maisha Allianz Arena
Video: Mkuu wa Mkoa Kagera awasha moto kwa watendaji wa vijiji