Meya wa Kinondoni, Benjamin Sitta amezindua mashindano ya Meya Cup ambayo hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kuinua vipaji vya vijana na kuwasaidia kuondokana na matatizo yanayowakumba.
Aidha, mashindano hayo yamezinduliwa katika Kata ya Msasani ambayo pia ni mashindano yanayoandaliwa na Chama cha Mapinduzi kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali.
“Mashindano haya ni ya kichama ambayo huwa yanaandaliwa na diwani anaekuwepo kwa kipindi husika, lengo ni kuokoa vipaji vya vijana,”amesema Sitta.
Hata hivyo kwa upande wake mratibu wa mashindano hayo, James Mwakibinga ameyaomba makampuni mbalimbali yaliyopo Jijini Dar es salaam kujitokeza na kudhamini mashindano hayo kwani yanalengo la kubua vipaji vya vijana.