Katika hali ya kuonyesha Kuunga Mkono juhudi zinazofanywa na Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli ya ‘hapa kazi tu’ na kuondoa watumishi ambao sio waaadilifu na wazembe,Mstahiki Meya wa kinondoni Mh.Boniphace Jacob leo amewafukuza kazi watumishi (4) wa afya na kuwasimamisha wengine na kushushwa madaraja ya vyeo kwa makosa mbalimbali.

Tukio hilo limetokea mapema hii leo alipokua akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam,Meya alisema kuwa uamuzi wa baraza la madiwani kuwapa onyo kali,kuwashusha madaraja na  kwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma,

Aidha baraza la madiwani limezingatia taratibu zote za sheria katika kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watumishi hao ambazo ni pamoja na kufanyika kwa uchunguzi wa awali kuhusu tuhuma husika na kufungua mashtaka dhidi yao.

Hata hivyo aliongeza kuwa baraza la madiwani lilipitia kwa kina mashauri yote ya kinidhamu na kujadili kwa kina na kuwapandisha vyeo watumishi 372’’ tumewabadili vyeo watumishi 9 na kuwadhibitisha kazini watumishi 206 ambao wamemaliza vipindi vyao vya majaribio’’ alisema bw, Jacob

JPM aanza kuinyoosha CCM
Serikali Yatoa Wito Kwa Taasisi Za Umma