Mwaka huu unaweza kuwa mwaka wa cheche kali za moto wa muziki ndani ya Afrika Mashariki, baada ya kuzinduliwa kwa tuzo kubwa zitakazowahusu wasanii wa nchi tano kati ya sita za Afrika Mashariki.
Tuzo hizo zilizobatizwa jina la Mseto East Africa Awards zilizinduliwa jana jijini Nairobi nchini Kenya, zikilenga kuwashindanisha wasanii wa ukanda huo kwenye vipengele 15, kuwapata malkia na wafalme waliofanya vizuri mwaka husika. Vipengele vya tuzo nyingine 10 vitakuwa maalum kwa nchi inayoandaa tuzo hizo mwaka huo.
Kwa mara ya kwanza, tuzo hizi zinaweka historia ya kuwa tuzo zinazofanyika kwa kuzunguka ndani ya nchi zote tano kwa kupokezana uandaaji, Tanzania, Uganda, Kenya, Burundi na Rwanda.
Dar24 ilimpata Lil Ommy, mtangazaji wa The Playlist ya Times FM ambaye alichaguliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye uzinduzi wa tuzo hizo jijini Nairobi, na alifunguka yaliyojili na joto litakaloletwa na tuzo hizo.
Angalia video hii kuipata: