Ofisi ya Takwimu nchini imesema kuwa hali ya mfumuko wa bei kwa kipindi cha Mwezi agosti umepungua hadi kufikia 4.9 ikilinganishwa asilimia5.1 kwa mwezi julai mwaka huu

Hayo yamesemwa Mkurugenzi wa sensa ya watu na takwimu za jamii nchini Ephraimu Kwesigabo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, amesema kuwa hali hiyo ya kupungua kwa bei za vyakula imetokana na upatikanaji wa bidhaa za vyakula sokoni .

”Kasi ya upandaji wa bei za vyakula imeshuka hii ni kutokana na huduma za vyakula kuongezeka sokoni na kusababisha upatikanaji wa bidhaa za vyakula kuwarahisi ”Alisema Kwesigabo”

Kwesigabo aliongeza kuwa wakati takwimu zikionesha mfumuko wa bei kushuka kwa asilimia 4.9 fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.28 kutoka asilimia 98.49 kwa kipindi cha mwezi Agosti mwaka huu .

Aidha Mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi agosti umezidi kupungua na kufikia asilimia 7.0 kutoka asilimia 7.6 kwa kipindi cha mwezi julai mwaka huu.
Tazama video hapa

Lipumba amvaa Lowassa, adai hatakubali ainunue CUF bei chee
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Seleman Jaffo Awataka Mgambo Kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu Kuto Wanyanyasa Mama Lishe