Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi James kilaba amesema kuwa mfumo wa TTMS unafaida kubwa katika nchi hasa kiuchumi.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam katika hafla ya makabidhiano ya mfumo huo, ambapo amezitaja baadhi ya faida hizo kuwa ni pamoja na uwezo wa mfumo huo kuhakiki mapato yote ya watoa huduma za mawasiliano na kugundua mawasiliano ya kughushi.
Amesema kuwa mfumo huo huwezesha upatikanaji wa takwimu za mawasiliano ya simu yanayofanyika ndani na nje ya nchi.
Aidha, ameongeza kuwa mfumo huo pia utasaidia kugundua mawasiliano ya simu ya ulaghai na kutambua mapato na takwimu za miamala ya fedha mtandaoni na kusimamia kwa ufanisi ubora wa huduma za mawasiliano na kusaidia kuboresha viwango vya huduma hizo.